Saturday, 25 July 2015

YANGA YANASA KIFAAA KIPYA

 0
Mshambuliaji wa Gor Mahia, Michael Olunga

Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga zinasema kwamba, mshambuliaji wake, Rais wa Liberia, Kpah Sherman anakaribia kutua katika klabu mojawapo inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Winga aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha  Yanga, Mbrazil,  Andrey Coutinho anatafutiwa timu itakayomnunua baada ya BDF XI ya Botswana kutaja pesa dau dogo la milion 10 za Kitanzania. Hata hivyo St.George ya Ethiopia wameonesha kuvutiwa na Coutinho.

Yanga imepanga kumalizana na kiungo mkabaji wa Gor Mahia , Khalid Auch pamoja na mshambuliaji Michael Olunga ambaye Azam FC na Simba SC wanawania saini yake pia.


Beki kiraka, Mbuyu Twite yupo mashakani kuendelea kukipiga Jangwani huku tatizo haswa imekuwa usumbufu kutoka klabu yake ya zamani ya FC LUPOPO.

PATA RATIBA YA KOMBE LA DUNIA HAPA

Thursday, 23 July 2015

CHELSEA YASAJIRI KINDA

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kumsajili mchezaji kutoka Club ya Partizan Belgrade anaitwa Danilo Pantic na kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Vittese

JAMAICA YAITOA USA CONCACAF

Timu ya taifa ya Marekani imeondolewa kwenye mashindano ya CONCACAF  baada ya jana kukubali kupokea kipigo cha mabao mawilikwa moja

BENTEKE RASMI LIVERPOOL

Club kongwe ya Liverpool imefanikiwa kumsajili mchezaji Aston Villa kwa ada ya pauni milioni 32.5 dili iyo ilikamilika jana baada ya mchezaji kufanyiwa vipimo vya afya

Wednesday, 22 July 2015

UNITED BADO WATAKA KUMSAJILI RAMOS


Manchester United wametuma ofa mpya Real Madrid wakiomba kumsajili Sergio Ramos, hii ni kwa mujibu wa Diego Torres wa gazeti la  El Pais.

Mwandishi huyo anayeishi Madrid, amedai kwamba United wameweka mezai Euro milioni 60 ili kumnasa Ramos, mshindi wa kombe la dunia 2010.

Man United wanaamini beki huyo ameshawishika kujiunga nao baada ya kutofautiana na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez.

Tayari United walishatuma ofa mbili kumsajili Ramos, lakini Madrid walikataa zote na ofa ya sasa inaweza kuwa ya mwisho.

United na Madrid wamekuwa wakivutana juu ya usajili wa Ramosi, huku miamba ya Bernabeu ikihitaji saini ya kipa wa Old Trafford, David De Gea.

Madrid tayari wamemsajili Kiko Casilla na wameonekana kukata tamaa kumpata De Gea mpaka majira ya kiangazi mwakani, hivyo United wanaona ni wakati wa kujaribu tena kumsajili Ramos.

MAN UNITED ,BARCELONA ZASHINDA MECHI ZA KILAFIKI


TAZAMA BARCELONA ILIVYOIPIGA LA GALAXY


UEFA CHAMPIONZ LIGI-PATA MATOKEO MARUDIANO RAUNDI YA PILI YA MTOANO



UCL-2014-15-LOGO-1JANA zilichezwa Mechi 9 za Marudiano ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, 
Mechi za hizo za Marudiano za Raundi ya Pili zitakamilika Leo na Washindi wake watatinga Raundi ya Tatu ya Mtoano ambayo tayari Droo yake imeshafanyika.
Washindi 15 wa Raundi ya Tatu ya Mtoano watacheza Raundi ya Mchujo, ambayo wataungana na Manchester United, Valencia CF, Bayer 04 Leverkusen, Sporting Clube de Portugal, na SS Lazio, ili kupata Timu 10 zitakazoingia Hatua ya Makundi ambayo ina Timu 22 ambazo zinaanzia hapo moja kwa moja wakiwemo Mabingwa FC Barcelona.
UEFA Championz Ligi
Raundi ya Pili ya Mtoano- Marudiano
Jumanne Julai 21
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi Mbili]
Dila Gori - Georgia 0 FK Partizan - Serbia 2 [0-3]
Pyunik FC - Armenia 1 Molde FK - Norway 0 [1-5]
FC Milsami - Moldova 2 Ludogorets Razgrad - Bulgaria 1 [3-1]
HJK Helsinki - Finland  1 FK Ventspils - Latvia 0 [4-1]
Maccabi Tel Aviv FC - Israel 5 Hibernians FC Paola - Malta 1 [6-3]
FK Vardar - Macedonia 1 Apoel Nicosia - Cyprus 1 [1-1]
Lincoln Red Imps - Gibraltar 0 FC Midtjylland - Denmark 2 [0-3]
Zalgiris Vilnius - Lithuania 0 Malmö FF - Sweden 1 [0-1]
Crusaders FC - Northern Ireland 3 Skenderbeu - Albania 2 [4-6]
Jumatano Julai 22
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
14:00 FC Astana - Kazakstan v NK Maribor - Slovenia [0-1]
18:00 Fola Esch - Luxembourg v NK Dinamo Zagreb - Croatia [1-1] 
18:30 Steaua Bucurest - Romania v AS Trencin - Slovakia [2-0]
18:30 Videoton Szekesfehervar - Hungary v The New Saints FC - Wales [1-0]
18:45 Dundalk FC - Ireland v FC Bate Borisov - Belarus [1-2]
18:45 Rudar - Montenegro v Qarabag Agdam FK - Azerbaijan [0-0]
18:45 KKS Lech Poznan - Poland v FK Sarajevo - Bosnia/Herzegovina [2-0]
19:15 Stjarnan - Iceland v Celtic - Scotland [0-2]

MAN UNITED PICHANI JINSI ILIVYOSHINDA NA SAN JOSE EARTHQUACK

The Dutch winger performed impressively and already has a good understanding with Wayne RooneyMemphis Depay slots the ball past San Jose goalkeeper David Bingham after collecting a loose back pass 

Tuesday, 21 July 2015

TUJIKUMBUSHE MACHESTER UNITED 2002/2003


NEWCASTLE UNITED YASAJIRI BONGE LA MSHAMBULIAJI

Timu ya Newcastle imefanikiwa kumsajili mshambuliaji raia Serbia kutoka katika klabu ya Anderlecht Aleksandar Mitrovc' ,mchezaji huyo mwenye miaka 20 alifanikiwa kufunga magoli 44 kwenye mechi 90 alizozichezea club yake hiyo ya zamani

 Akizungumza baada ya kukamilisha usajili wake huo mchezaji huyo amesema "najisikia mwenye furaha kuwa hapa Newcastle ni timu kubwa na ni fahari kuwa hapa


Aleksandar Mitrović
Aleksandar Mitrović
Date of Birth:16 Sep 1994 (Age 20)
Place of Birth:Smederevo
Nationality:Serbia
Height:189 cm.
Weight:87 Kg.
Position:Striker
Squad Number:

AZAM YAFANYA KWELI

Matajiri wa jiji la Dar es salaam, Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini katika mechi ya pili ya kombe la Kagame iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa, Dar es salaamMagoli ya Azam yamefungwa na nahodha mwandamizi wa klabu hiyo, John Raphael Bocco 'Adebayor' katika dakika ya 27' na Kipre Herman Tchetche dakika ya 52.Hili ni goli la pili la Bocco kwani mechi ya kwanza dhidi ya KCCA ya Uganda, Straika huyo wa Taifa Stars, alifunga goli pekee katika ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya ufunguzi ya Kagame Cup iliyopigwa juzi uwanja wa Taifa.Kwa matokeo hayo, Azam FC wamefikisha pointi sita na kuwa na uhakika wa asilimia 100 kutinga robo fainali. 


LEO TUNAJIKUMBUSHA KIDOGO CHELSEA 2014 ILIVYOCHUKUA UBINGWA


WAWANIA TUZO MCHEZAJI BORA ULAYA WATAJWA KUMI BORA

Shilikisho la soka barani ulaya limetangaza majina kumi yanayowania mchezaji bora wa dunia ambayo ni

RONADRO CHRISTIAN

NEYMER

MESS

TEVES

PILRO

VIDAL

HAZARD

BUFFON

SUAREZ

POGBA

STAMBOULI TAYARI KATUA PSG

Kablu ya PSG ya Ufaransa imefanikiwa kumsajili mchezaji wa tottenham spurs Stamboul kwa ada ya paun million 8

VIDALI KUTUA BAYERN MUNICH

Mchezaji wa juventus Aturo Vidal anatarajiwa kusaini kwa mabingwa mara tatu wa ujerumani bayern munich kwa munich kwa ada ya kiasi cha euro milion 40

Rais wa juventus MORRATA amesibitisha ilo kwamba makubaliana tayari kinachosubiliwa ni mchezaji kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mikataba binafsi na klabu yake iyo mpya
\
Vidal is leaving Juventus, confirms Marotta

Monday, 20 July 2015

KUMBUKUMBU YA LEO

RONALDINHO ASAJILIWA BARCELONA 2003

BENTEKE KUFANYAVIPIMO VYA AFYA LEO

Mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke anatalajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo hii tayari kwa kujiunga na majogoo wa LONDON kwauamisho wa paun milioni 32.5

 Christian Benteke celebrates his equaliser against Liverpool in the FA Cup Semi-Final match, 2015

All Afrika Games CAF yataja makundi

Twiga stars mazoezini
Upangaji wa makundi wa soka ya wanawake ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika nchini Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-19 umefanywa na Shirikisho la soka barani Afrika, CAF na timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Kongo, Nigeria na Ivory Coast.
Upangaji wa makundi hayo umefanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.
Kundi B lina timu za Cameroon, Afrika Kusini, Ghana na Misri. Upande wa wanaume, Kundi A lina timu za Kongo, Sudan, Zimbabwe na Burkina Faso, wakati Kundi B kuna Ghana, Senegal, Misri na Nigeria 

MESSI AZINDUA UWANJA GABON


Messi azindua uwanja wa kombe la mataifa ya Afrika 2017 Gabon
Mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani mara nne ,Lionel Messi, amekutana na rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba.
Mchezaji wa Argentina na mabingwa wa ligi kuu ya Ulaya Barcelona aliweka jiwe la msingi la uwanja utakaotumika kuandaa mechi za fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2017.
Mchezaji huyo maarufu wa kilabu cha Barcelona ,mshindi wa tuzo la Mfalme wa Uhispania Copa del Rey na ligi ya Ulaya msimu uliopita,alizindua rasmi mchakato wa ujenzi katika uwanja wa soka wa Port-Gentil.
Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika kwenye eneo kubwa la mchanga ambapo uwanja huo wa soka utajengwa.
Ni ziara ya kwanza ya mshambuliaji huyo wa Argentina nchini Gabon na aliweka saini yake kwenye jezi zinazovaliwa na mashabiki wake , kabla ya kuweka jiwe la msingi akiambatana na rais.
null
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000
" Nilipokua Barcelona miaka michache iliyopita , nilikutana na Messi ambaye aliniambia kwamba atakuja kunitembelea mjini Libreville," alisema rais wa Gabon.
" Ni ahadi aliyonipa.''
''Ni mtu anayetimiza ahadi ."
Uwanja huo mpya utakua na uwezo wa kuwapokea mashabiki 20,000 na unatarajiwa kuandaa mechi kuanzia mwezi Novemba 2016 katika michezo ya awali ya shindano hilo.

Blatter atupiwa pesa Zurich

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ametupiwa pesa na mtu aliyevamia mkutano wake na wanahabari.
Mvamizi huyo aliyetambuliwa kama Lee Nelson raia wa Uingereza aliondolewa ukumbini humo mara moja na maafisa wa usalama wa FIFA.
Blatter aliyekuwa ameudhika sana na tukio hilo alisema 'halikuhusiana kwa njia yeyote na kandanda' kabla yake kuondoka ukumbini.
Blatter alitangaza mabadiliko kadha ikianza na tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa mwezi Februari mwakani.
null
Mvamizi huyo aliyetambuliwa kama Lee Nelson ni raia wa Uingereza
Aidha Viongozi watakaokuwa na ari ya kurithi kiti hicho cha rais wa FIFA,sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi lake la kuwa rais wa FIFA.
Mkutano huo wa leo pia ulitaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kuweka kikomo cha muhula cha urais na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo.
null
Aidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi
Hatua ya kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo pia ilijadiliwa.
Aidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi wa kina kubaini njia za kukabiliana na rushwa na ubadhirifu.
Jopo hilo maalum ndilo litakaloendesha m

FIFA kuchagua rais mpya Februari 2016

Shirikisho la soka duniani Fifa litaandaa kongamano la dharura kuchagua rais mpya tarehe 26 mwezi februari mwakani.
Hii ni licha ya rais aliyeko sasa Sepp Blatter kutangaza nia ya kuondoka mamlakani wiki moja tu baada ya kuchaguliwa upya kuwa rais wa shirikisho hilo tarehe 26 mwezi Mei.
Tangazo hilo lilifuatia juma lenye matukio na madai ya ulaji rushwa na ufisadi miongoni mwa maafisa wakuu wa FIFA.
Viongozi watakaokuwa na ari ya kurithi kiti hicho cha rais wa FIFA,sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi lake la kuwa rais wa FIFA.
FIFA inatarajiwa kuandaa mkutano na waandishi wa habari muda mchache ujao.
null
Wagombea kiti cha Urais sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Kufikia wakati wa uchaguzi huo mpya Blatter atakuwa tayari keshahudumu kwa miezi tisa tangu atoe tangazo la kujiuzulu kufuatia shtuma kali za ufisadi dhidi ya shirikisho na haswa maafisa wakuu wa FIFA.
Mapema hii leo mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo wa mwezi Mei, mwanamfalme kutoka Jordan Prince Ali bin al-Hussein alimtaka kiongozi huyo mswisi kunga'tuka mamlakani mara moja.
Mwanamfalme al-Hussein,alisema ''Blatter lazima ajiuzulu na aondoke mara moja''
null
Prince Ali bin al-Hussein alimtaka kiongozi huyo mswisi kunga'tuka mamlakani mara moja
Haifai aendelee kuingoza FIFA.
Tume maalum iundwe na ipewe mamlaka ya kusimamia uchaguzi mkuu wa FIFA .''aliongezea Prince al-Hussein.
Mkutano huo wa leo pia unatarajia kutaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kuweka kikomo cha muhula cha urais na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo.
Hatua ya kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa juu wa shirikisho hilo pia itajadiliwa.

LIVERPOOL MPYA NDIO HII YAPIGA MTU AUSTRALIA

ARSENA VS EVERTON HIGHLIGHT

WALE NAO HAWAKUONA MECHI YA ASERNAL NA EVERTON ASIAN CUP

matukio MAN UNITED VS CLUB AMERICA



kwa wale ambao hawakuangalia mechi ya united na club america video ikionyesha matukio ya mechi ilivyokua 

JEZI MPYA YA MANCHESTER UNITED YA MSIMU UJAAAO IMELIKI

KUHUSU MUSTAKABARI WA SARAH MOULIHNO ANENA


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amethibitisha kuwa wachezaji wake wawili, Mohamed Salah na Filipe Luis wataruhusiwa kuondoka klabuni hapo endapo wataletewa ofa nzuri kwa ajili ya kuwauza wacheza hao.
Luis alisajiliwa kutoka Atletico Madrid msimu uliopita kwa ada ya pauni milioni 15.8, lakini ameshindwa kuonesha makali yake huku pia akihusishwa kurudi katika klabu yake ya zamani yenye maskani yake Vicente Calderon, japokuwa Mourinho amesema hali hiyo itatokea endapo ofa nzuri italetwa.
Wakati huohuo, mustakabali wa Salah pia uko mashakani baada ya kukuataa kuongeza muda wake wa mkopo kukaa katika klabu ya Fiorentina, huku Roma wakisemekana kuwa mbioni kumwania mchezaji huyo, kutokana na ukweli kwamba Mourinho amekiri kuwa nyota huyo wa M isri hana tena nafasi katika kikosi chake
"Kama wanamuhitaji basi wanatakiwa watupe hela na pia tujadili ofa yao kama ni nzuri", Mourinho aliwaambia waandishi". Halafu baada ya hapo tunatakiwa kuingia sokoni haraka iwezekanavyo.
"Naona mustakabali wa Salah kwingine kabisa, iwe ama kwa mkopo au iletwe ofa ili tumuuze. Kwa wakati huu ambapo tuna Hazard na Willian, Traore, Moses na Cuadrado, tuna takribani wachezaji 5 katika nafasi hizi. Ni vyema kama hatutakuwa nao weng