VPL Team of the Week: Bahanuzi, ndemla, Yondani wote ndani




Goal inakuletea timu ya wiki baada ya michezo iliyopigwa wiki hii katika viwanja mbalimbali
1.Ally Mustaph ‘Barthez’
Kipa wa Yanga ambaye alifanya kazi kubwa Jumamosi ya kuzuia mashambulizi wa washambuliaji wa Simba na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0, kwenye mechi ngumu yenye ushindani anapata 11.
2.Michael Aidan
Beki wa JKT Ruvu ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo licha ya kuwa na matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu huu ndiye aliyeipa presha Stand United na kushindwa kulishambulia lango lao kwa muda mrefu licha ya bao la dakika za mwishoni anapata 2.
3.Hassan Mwasapili
Beki wa kushoto wa Mbeya City ambaye licha ya timu yake kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Azam FC, lakini alicheza vizuri na kutoa mchango mkubwa kwa timu yake na ndiye aliyechangia timu hiyo kupata bao la kufutia machozi anapata 3.
4.Kelvin Yondan
Beki mahiri wa kati aliyetoa mchango mkubwa kwa Yanga iliyopata ushindi wa mabao 2-0 Jumamosi dhidi ya wapinzani wao Simba Yondan tofauti na mechi nyingine za Simba na Yanga katika mechi ya juzi alicheza kwa kiwango cha juu kuipa timu yake ushindi anapata 4.
5.Pascal Wawa
Beki wa kati wa Azam FC, ambaye ameendelea kutoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Stewart Hall, beki huyo raia wa Ivory Coast, amekuwa chachu ya matokeo wanayoyapata Azam tangu kuanza kwa msimu huu anapata 5.
6.Awadh Juma
Kiungo wa Simba ambaye alifanya vizuri na kuisaidia timu yake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga, Awadhi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake kwa kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga na kusaidia mashambulizi na kunawakati alipoteza nafasi ya wazi dakika za mwishoni anapata 6.
7.John Mahundi
Winga wa kulia wa Mbeya City,amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake licha ya matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Azam FC, winga huyo anapata 7.
8.Said Ndemla
Kiungo wa Simba ameendelea kubaki kwenye kikosi bora cha wiki kama ilivyokuwa wiki iliyopita Ndemla, alifanya vizuri kwenye mechi ya Jumamosi wakati timu yake ilipocheza na Yanga na kufungwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa taifa anapata 8.
9.Amissi Tambwe
Mshambuliaji hatari raia wa Burundi ameendelea kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Yanga baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wan ne mfululizo Jumamosi kwa kuifunga Simba timu ambayo aliichezea misimu miwili iliyopita kabla ya kuhamia Yanga kwenye dirisha dogo msimu uliopita anapata 9.
10.Said Bahanuzi
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar ameanza kuonyesha makali yake akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar mchango wake uliisaidia timu hiyo kupata ushindi wan ne mfululizo Jumamosi wakati walipoifunga Majimaji ya Sokongea bao 1-0 anapata 10.
11.Twaha Shekuhe
Winga wa Wagosi wa Kaya Coastal Union ya Tanga amerejea kwenye kiwango chake na kuipigania timu yake ya Coastal ingawa mambo bado si mazuri kwa timu hiyo anapata 11.