Friday, 13 January 2017

Diego Costa kutemwa kikosi kitakachoumana na Leicester city leo

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji nyota Wa timu ya taifa ya Spain na kilabu cha Chelsea Diego Costa ataukosa mchezo Wa Leo ambapo Chelsea watakuwa wageni dhidi ya mabingwa watetezi Leicester city. Imeripotiwa kutokea kwa kutoelewana au kugombana kwa mshambuliaji huyo na kocha anayekinoa kikosi icho Antonio Conte pamoja na fitness coach Julio Tous.

Diego Costa aliripoti kuwa na maumivu ya mgongo ila timu ya madaktari walipuuza malalamiko yake yaliyopelekea mshambuliaji huyo kugomea mazoezi huku kocha wake kuamua kuwa upande wa jopo la madaktari kuwa kinyume na maamuzi ya mshambuliaji huyo anayesifika kwa utata katika vitendo..

Aidha Uongozi Wa Chelsea umekataa kutoa taarifa yoyote juu ya kusambaa kwa suala la mshambuliaji huyo kutemwa katika kikosi kinachoanza Leo.


Ripoti hizi huenda zikachochea tetesi za mshambuliaji huyo kutaka kuondoka katika kilabu icho na kutimkia ligi kuu ya uchina ambapo kandarasi yake imekua katika uhitaji mkubwa licha ya Conte kutaarifu kuwa biashara kati ya kilabu icho na uchina imekwisha kwa sasa.

Diego Costa ameweka kambani mipira 14 na kusaidia upatikanaji Wa magoli mengine 5 ka



Sunday, 8 January 2017

Wayne Rooney afikia Rekodi ya mabao ya legendary Sir Bobby Charlton

Mshambuliaji nyota Wa kilabu cha Manchester United na timu ya taifa ya uingereza, Wayne Rooney sasa anahitaji bao moja kuwa mfungaji bora Wa muda wote wa timu hiyo baada ya jana kufikia record ya mabao 249 akiwa na jezi ya Manchester united hapo Jana katika michuano ya raundi ya 3 ya FA walipoumana na kilabu cha reading.

Awali Wayne Rooney amepita akivunja records za Dennis Viollet (179 goals), Jack Rowley (211 goals), Denis law (237 goals), na kwa sasa hakuna mchezaji mwingine amefunga mabao mengi zaidi take katika kilabu icho.