Rayo waliongoza 2-0 ndani ya Dakika 14 kwa Bao Adrián Embarba na Ladislao “Miku” Fedor lakini Real wakajikongoja na kufunga Bao la kwanza kupitia Gareth Bale na kusawazisha kupitia Lucas Vázquez alieingizwa kumbadili Karim Benzema alieumia.
Bale ndie alieipa Real ushindi kwa kufunga Bao la 3 zikibakika Dakika 9 Mpira kwisha.
MAGOLI:
Rayo Vallecano 2
-Adrian Embarba 7
-Nicolas Fedor Miku 14
Real Madrid 3
-Gareth Bale 35
-Vazquez Lucas 52
-Gareth Bale 81
Ushindi huu umewaweka Real wakiwa kileleni mwa La Liga Pointi 2 mbele ya Barcelona na Atletico Madrid ambbazo zitacheza Mechi zao za mkononi baadae Usiku huu.