Saturday, 7 January 2017

Kwa nini nyota Aubameyang alihudhuria 2017 CAF awards ceremony akiwa na mavazi yasio Rasmi?

Nyota mshambuliaji Wa kilabu cha Borrusia Dortmund cha ujerumani na timu ya taifa ya Gabon juzi alihushuria hafla za utoaji tuzo za wachezaji nyota Wa afrika nchini Nigeria,Abuja akiwa amevalia mavazi ya "Bash" .

Hiyo ni kutokana na kupotelewa na mizigo yake alipotua katika airport ya Abuja. Pierre Emeric Subameyang usiku huo alishuhudia nyota wa Leicester city na timu ya taifa ya Algeria Riyaad Mahrez akitwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha kilabu chake kushinda taji la Bacleys premier league ya Uingereza.

Tukio hilo lilitokea ikiwa imebaki takribani wiki 1 kuanza kwa michuano ya mataifa huru ya Africa AFCON nchini Gabon.

Wenger akiri angeweza kumtumia kiungo Jack Wilshere kwa sasa

Manager Wa washika mitutu Wa London, arsené Wenger amekiri angeweza kumtumia kiungo mwingereza Jack Wilshere katika kikosi chake cha sasa kilichokumbwa na majeruhi.
Jack wilshere alipelekwa kwa mkopo Wa mda mrefu katika kilabu cha Bournemouth mnamo mwezi Wa August ambapo mpaka sasa ameonesha uwezo mzuri.

Arsenal kwa muda mrefu sasa inakosa huduma ya kiungo wake mahiri Santiago carzola pamoja na mfaransa fransis Coquelin ambaye atakosekana kwa takribani wiki nne.

Alipoulizwa kama angeweza kumtumia Jack kwa sasa alijibu "ndio ningeweza kumtumia sasa"

"Lakini kama angekua hajacheza match yoyote mpaka sasa pia asingekuwa tayari kucheza kwa sasa. Na mpaka sasa naona ilikua uamuzi sahihi kwake kuenda kukipiga Bournemouth kwa mkopo"


Wilshere ambaye amecheza michezo 17 (15 akiwa na Bournemouth) ni idadi kubwa kwake ya michezo tangu msimu Wa 2013-2014

Arsenal Leo inajitupa dimbani kukipiga na Preston North end katika michuano ya FA ya pale uingereza

angalia magori kumi bora ya scorpion kick


Friday, 6 January 2017

hatimaye Arsenal yasajiri dilisha dogo

klabu ya arsenal imefanikiwa kumsajili mchezaji kinda kutoka klabu ya mtaani Hednseford ,mcheji huyo anaitwa Bramall na anauwezo wa kucheza beki zote mbili za pembeni

arsenal ilituma maskauti wake ili kuchunguza vizuri kwa muda wa miezi mitatu na baadae kulizishwa na kiwango chake hivyo kuamua kumsajili na kumpeleka mojakwa moja kwenye kikosi cha U20

morgan schneiderlin na depay wanaweza kuondoka mourihno asema

kiungo mkabaji wa manchester united morgan schneiderlin pamoja na kiungo mshambuliaji wa united memphis depay wanaweza kuondoka wakati wowote kama offa staiki itatokea ,
hao yamesemwa na kocha wa mashetani wekundu man united wakati wa press conference kuelekea katika mchezo wa kombe la FA wakicheza na Reding inayonolewa na beki kisiki wa zamani wa united jap stam

"hali yao iko sawa kwa wote wawili ,na nitawaruhusu kuondoka kama ofa sahihi itatokea lakini mpaka sasa hapana offa yoyote ,
je ni vizuri? hapana kwa nn hapana ?kwa sababu siwafikilii tena kama ni wachezaji  mbadala kwenye kikosi changu .Kwa kawaida ningewachagua kwa mechi ya kesho lakini hapana kwa sababu tunasubiria kitu ambacho kwa wiki chache zilizopita kilikuwa 100% lakini si kwa sasa"  alisema mourihno

lakini pia wachezaji hao wanahusishwa na kutua kwa mkopo katika klabu ya Everton


Thursday, 5 January 2017

chelsea hoi kwa tottenham spurs

Timu ya chelsea jana iliambulia kipigo cha tatu kwa msimu huuu na cha kwanza baaada y akutofungwa karibia mechi kumi na tatu (13) ,

mabao mawili  yaliyofungwa na kiungo mshambuliaji Delle Ally yalitosha labisa ndoto za chelsea kuweka rekodi na kuzidi kujikita kileleni ,mwa ligi na ivyo kufanya nafasi ya kugombania kombe kuwa wazi kwa kila upande kwa zile timu zote sita zilizo juu ,


 Tottenham's Dele Alli scores their first goal
 Ally akifunga goli la kwanza mbele ya mabeki wa chelsea