Saturday, 7 January 2017

Wenger akiri angeweza kumtumia kiungo Jack Wilshere kwa sasa

Manager Wa washika mitutu Wa London, arsené Wenger amekiri angeweza kumtumia kiungo mwingereza Jack Wilshere katika kikosi chake cha sasa kilichokumbwa na majeruhi.
Jack wilshere alipelekwa kwa mkopo Wa mda mrefu katika kilabu cha Bournemouth mnamo mwezi Wa August ambapo mpaka sasa ameonesha uwezo mzuri.

Arsenal kwa muda mrefu sasa inakosa huduma ya kiungo wake mahiri Santiago carzola pamoja na mfaransa fransis Coquelin ambaye atakosekana kwa takribani wiki nne.

Alipoulizwa kama angeweza kumtumia Jack kwa sasa alijibu "ndio ningeweza kumtumia sasa"

"Lakini kama angekua hajacheza match yoyote mpaka sasa pia asingekuwa tayari kucheza kwa sasa. Na mpaka sasa naona ilikua uamuzi sahihi kwake kuenda kukipiga Bournemouth kwa mkopo"


Wilshere ambaye amecheza michezo 17 (15 akiwa na Bournemouth) ni idadi kubwa kwake ya michezo tangu msimu Wa 2013-2014

Arsenal Leo inajitupa dimbani kukipiga na Preston North end katika michuano ya FA ya pale uingereza

No comments:

Post a Comment