Friday, 27 May 2016

HATIMAYE YAMETIMIA MOURIHNO TO UNITED






Manchester united leo wamesibitisha rasmi kuwa Kocha mourihno amesain mkataba wa kuifundisha united kwa muda wa miaka mitatu na wanyongeza kama atataka kuendelea kuifundisha united tena na antazamiwa kupoa mshahara wa pauni milioni 15 kwa mwaka ,kwa habari zaidi

We are delighted to announce Jose Mourinho is our new manager! Full statement: http://bit.ly/22r1xOq#WelcomeJose

Wednesday, 25 May 2016

Mourihno aaanza kuchokonoa wenga

Imebaki kidogo tu man united wamtangaze jose mourinho kama kocha wao ,nae inasemekana kuanza mipango yake ya usajili na tayari ameanza kutupia macho beki tegemeo wa Arsenal kocsienly na kusema anataka kumsajili na kumpeleka united

Arsenal Wakamilisha usajili wa kwanza

Arsenal wakamilisha usajili wa Granit Xhaka kutoka Borussia Monchenglabach kwa ada ya kiasi cha paun millio 33.1,
mchezaji huyo amefanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha dili lake na atavaaa jezi namba 34 iliyokuwa inavaliwa na cocoline ambaye amekubali kubadilisha jezi yake

'nafurahi kujiunga na Arsenal ni timu nzuri na naaamini nitatimiza ndoto zangu hapa " alisema mchezaji huyo


Tuesday, 24 May 2016

BARTON KATUA RANGERS FC

kiungo mtukutu wa uingeleza JOE BARTON ajiunga na RANGERS FC ya Scotland mchezaji huyo ambaye ana miaka 33 amekubali kujiunga na timu iyo akitokea katika timu ya bunlery ambaya ina pambana kurudi katika ligi kuu

'ni maamuzi magumu sana kuama england asa katika kipindi hiki kigumu amba timu yangu inapambana kuingia kati ligi kuu msimu ujao lakini sina cha kufanya zaidi kuacha maisha yaendelee kama yalivyo ' alisema mchezaji huyo


MOULIHNO HUYO UNITED

MABINGWA WAPYA wa FA CUP Manchester United wanatarajiwa wakati wowote saa 24 zijazo kumtangaza   Jose Mourinho kuwa Meneja wao mpya.
Habari hizi zimepamba moto kwenye Ulimwengu wa Soka lakini, kama kawaida yao, Klabu ya Man United haijatoa tamko lolote.
Jana Meneja wa sasa Louis van Gaal aliiongoza Timu yake huko Wembley Stadium Jijini London kubeba kwa mara ya 12 FA CUP walipoichapa 2- 1 Crystal Palace kwa Bao la ushindi la Dakika ya 110 la Jesse Lingard ambalo lilifungwa huku Man United wakiwa Mtu 10 baada ya Chris Smalling akiwa ametolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 105 lakini alitimuliwa siku mbili baadae
Licha ya ushindi huo, kule kukosa Nafasi ya kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI ndiko kunaonekana kutamgharimu Van Gaal Umeneja kama vile alivyotimuliwa David Moyes Mwaka 2014.
 Van Gaal na Mourinho walishawahi  kufanya kazi pamoja kwani walikuwa pamoja huko FC Barcelona wakati Van Gaal akiwa Kocha Mkuu na Mourinho Msaidizi wake.
Wawili hao wanasemekana ni Maswahiba wazuri tu.
 MOU-OLDTRAFFORD

AZAM, YANGA KUTIMUANA KESHO FA NKONGO KATIKATI

Mwamuzi mahiri nchini, Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, Jumatano Mei 25, 2016 ameteuliwa kuwa mwamuzi atakayechezesha mchezo wa fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayozikutanisha timu za Young Africans na Azam FC; zote za jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza kesho saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand Chancha wa Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia. Kamishna wa mchezo huo anatakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu msimu 2015/16, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu 2015/16 wataiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17. Nafasi hiyo imechukuliwa na Young Africans.
Kadhalika Azam ina tiketi tayari ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kufika fainali za ASFC ingawa kanuni zinataka bingwa ambako kwa upande wa Yanga wana tiketi ya michuano ya juu zaidi ya shirikisho. Mvuto wa mchezo wa Jumatano ni ushindani wa soka na zawadi kwa bingwa.
Fainali za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).

Mourihno kutua na Ibra kadabra United

SUPASTAA wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ameripotiwa kuwa ameaafikiana na Manchester United kujiunga nao kwa Mkataba wa Mwaka mmoja na huenda akawa ndie Mchezaji wa kwanza kabisa kusainiwa na Jose Mourinho ambae anategemewa wakati wowote ule kuanzia sasa kutangazwa ndie Meneja mpya.
Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, anategemewa kusaini Mkataba huo wa Mwaka mmoja wenye kipengele cha nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi akiwa Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Paris Saint-Germain.
Msimu huu huko France, Ibrahimovic aliipigia PSG Bao 38 na kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa Taji la Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo.
Mourinho anategemewa kumrithi Louis van Gaal alieondolewa Jana na hilo linaonekana ndilo limemshawishi Ibrahimovic kujiunga na Man united.
Mourinho na Ibrahimovic walikuwa pamoja huko San Siro wakati Inter Milan inapata mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kutwaa Trebo ikiwemo UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2010 wakiifanya inter kuwa Klabu ya kwanza huko Italy kutimiza hilo.
Wawili hao wamekuwa na uhusiano mzuri mno kiasi cha Ibrahimovic kuandika kwenye Kitabu cha Maisha yake kwamba: “Mourinho anaweza kuwa Mtu ninaeweza kuwa tayari kufa kwa ajili yake!”
 Manchester United and Mourinho set to offer £34m deal to Ibrahimovic

RATIBA YA KUNDI A || MECHI ZA YANGA


- MO Bejaia vs Young Africans (17 June 2016)
- Young Africans vs TP Mazembe (28 June 2016)
- Young Africans vs Madeama (15 July 2016)
- Madeama vs Young Africans (26 July 2016)
- Young Africans vs MO Bejaia (12 August 2016)
- TP Mazembe vs Young Africans (23 August 2016)
Taarifa kutoka Website ya CAF - Afrika