Na Saleh Ally
IDADI
kubwa ya wadau wa soka hapa nyumbani Tanzania, England na kwingineko
duniani wanajiuliza swali moja tu muhimu. Kweli Manchester United
itakubali kuwa ngazi, ipigwe na Leicester City iwe bingwa wa England kwa
mara ya kwanza?
Kama
Leicester ambayo iko ugenini kesho kwenye Uwanja wa Old Trafford
itashinda dhidi ya Man United, basi itakuwa imefikisha pointi 79 tofauti
ya pointi 10 dhidi ya Tottenham Hotspur ambao wanashika nafasi ya pili.
Kama
ni hesabu, inaonekana hivi, ni lazima Leicester watakuwa mabingwa wa
England msimu huu. Kama ni miujiza, basi ina uwezo wa kuwazuia kwa
asilimia 10 pekee, kwa kuwa mpira nao hauaminiki.
Lakini
kusema lazima watakuwa mabingwa, bado inawezekana kwa asilimia 90.
Kwani hata kama kesho watapata sare dhidi ya Man United, bado wanaweza
kutangazwa mabingwa rasmi keshokutwa Jumatatu kama Tottenham watapoteza
mchezo wao dhidi ya Chelsea wakiwa ugenini Stamford Bridge.
Hata
hivyo, bado mechi ya kesho ndiyo inabaki kuwa kila kitu kwa Leicester
ambao kama watabeba ubingwa, basi ni wachezaji hadi kocha watakuwa
wameweka rekodi na kufanya mabadiliko huku wakiweka kumbukumbu ya
Blackburn Rovers iliyopanda daraja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England
msimu wa 1994-95.
Mechi zilizopita:
Manchester
United haina nguvu ya kufukuzana na Leicester kama utazungumzia ubingwa
lakini katika mechi zake sita zilizopita, imeshinda nne na kupoteza
mbili. Leicester imeshinda tano na sare moja.
Kwa
mwendo, Leicester wako vizuri zaidi lakini kamwe hauwezi kuwabeza Man
United kwa kuwa mwishoni kikosi chao kinaonekana kuwa vizuri zaidi na
wamefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la FA.
Ugenini:
Leicester
ni kati ya timu bora zinapokuwa zinacheza ugenini. Kwani kati ya
michezo 12, imeshinda mechi 10, imetoka sare 1 na kupoteza 1. Hii inaipa
asilimia 71 za ushindi inapokuwa nje ya nyumbani.
Hivyo
katika pointi zake 67 katika msimamo sasa, 31 imefanikiwa kukusanya
ikiwa ugenini. Hili si jambo dogo na Man United hawapaswi kuibeza
Leicester hiyo kesho.
Kwa
Manchester United, wakiwa nyumbani inaonekana hivi; katika mechi 11,
wameshinda 11 bila sare au kupoteza. Maana yake wana asilimia kubwa
zaidi ya kufanya vizuri nyumbani.
Mechi hii itakuwa burudani ya aina yake na huenda ikawa gumzo kwa kuingia kwenye historia ya soka la England.
Presha:
Katika
mechi hiyo, wanachotaka Manchester United ni kupata nafasi ya kucheza
Ligi ya Mabingwa Ulaya, yaani Top Four, japokuwa bado watakuwa hawataki
kugeuzwa ngazi hiyo kesho na kuingia kwenye historia kuwa wa mwisho
‘kuisaidia’ Leicester kuwa bingwa.
Kwa
Leiceter, lazima watakuwa kwenye presha kubwa kidogo ambayo inaweza
kuwa msaada au tatizo kwao. Kuwa mabingwa ni jambo ambalo wana hamu
kubwa, pia wana hofu kuu ya kufungwa. Haya wakiyachanganya vibaya,
huenda yatawaangusha na wakashindwa kucheza mpira wao.
Mechi 5:
Katika
mechi tano za mwisho ambazo Man United imecheza. Imefanikiwa kufunga
mabao manne ikafungwa matatu wakati ilipopoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya
Tottenham. Man United inaonekana iko makini kwenye ulinzi, lakini
ikiotewa, kweli inalainika.
Leicester,
mechi zao tano wamezicheza hivi, wameshinda mabao tisa, wakaruhusu
mabao manne. Aina ya uchezaji inaonekana ni ‘open game’. Mchezo ambao si
wa ulinzi mwingi sana na wanaweza kukufunga mabao mengi ukizubaa lakini
wanafungika.
Mara ya mwisho:
Mara
ya mwisho zilikutana Novemba 28, mwaka jana ikiwa ni mechi ya mzunguko
wa kwanza wa Ligi Kuu England. Matokeo yalikuwa 1-1 licha ya Man United
iliyokuwa ugenini kwa bao la kusawazisha la kiungo Mjerumani Bastian
Schweinsteiger.
Hii
inaonyesha hata mechi ya kesho, haitakuwa rahisi kwa kila timu. Ingawa
Leicester lazima wacheze wakitaka ushindi hata kama sare inaweza kuwapa
ubingwa.
Wanakosekana:
Kila
upande utakosa watu muhimu, wageni Leicester kama kawaida, mshambuliaji
wao nyota Jamie Vardy anaendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa.
Walimkosa katika mechi iliyopita dhidi ya Swansea, lakini wakashinda 4-0
wakiongozwa na Riyad Mahrez.
Manchester
nao wana kazi kidogo, wanaendelea kuwakosa wachezaji kama
Schweinsteiger aliyewakomboa wakiwa ugenini dhidi ya Leicester. Pia Luke
Shaw, Will Keane na Adnan Januzaj nao wanakosekana. Hawawezi kuwa
athari kubwa kwa Man United kwa kuwa wamekuwa nje kwa mechi kadhaa na
imeendelea kupambana.
Wabetishaji:
Kampuni
nyingi za kubeti za England zinaonekana kutoa nafasi kubwa kwa Man
United kushinda mechi hiyo, wakiamini presha kubwa itawamaliza
Leicester.
Inaonekana
wanaocheza mchezo huo, wengi wamechanganyikiwa, lakini wahusika wakuu,
wamewapa nafasi Man United kwamba wana nafasi kubwa kutokana na mwendo.
Ingawa wafanyabiashara wa ubetishaji, pia ni wajanja wanaweza kulalia wanakoona, kutaharibika ili kutengeneza biashara yao.