IFUATAYO ni Taarifa inayofafanua hali halisi:
-BPL, LIGI KUU ENGLAND na Nafasi zake kucheza Klabu Ulaya:
England ina Nafasi 4 [Inaweza zikawa 5] kwenye UCL na 3 kwenye EUROPA LIGI.
Bingwa wa BPL ataingia moja kwa moja Hatua ya Makundi ya UCL pamoja na Mshindi wa Pili na wa Tatu.
Atakaemaliza Nafasi ya 4 ataanzia Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UCL ambayo husaka Timu za kuingia Hatua ya Makundi.
Bingwa wa FA CUP atacheza Hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI na Bingwa wa Kombe la Ligi, Capital One Cup, atacheza Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya EUROPA LIGI.
Ikiwa Bingwa wa sasa wa Kombe la Ligi, Man City, watafuzu kucheza UCL Msimu ujao basi Nafasi yake ya kucheza EUROPA LIGI itakwenda kwa Timu moja itayomaliza Nafasi ya juu kwenye Msimamo wa BPL [Fuatilia ufafanuzi zaidi chini].
-Uwezekano wa Timu 5 za BPL kucheza UCL:
Hili litawezekana ikiwa Liverpool watabeba EUROPA LIGI na pia kumaliza nje ya 4 Bora ya BPL.
-Uwezekano wa Timu ya 4 ya BPL kutocheza UCL:
Ikiwa Manchester City watabeba Ubingwa wa UCL na kumaliza Nafasi ya 4 kwenye BPL basi wao watatetea Ubingwa wao wa UCL kuanzia Hatua ya Makundi na hakuna Timu nyingine itayochukua Nafasi yake ya 4 ya BPL kucheza UCL.
Ikiwa City watatwaa UCL na kumaliza nje ya 4 Bora za UCL basi ile Timu ya 4 ya BPL itapelekwa kucheza EUROPA LIGI.
-Nafasi 3 za kucheza EUROPA LIGI:
Kucheza EUROPA LIGI katika Hatua za Makundi hufuatia Nafasi Timu iliyomaliza kwenye BPL kama inavyoelezwa chini, au kutwaa FA CUP huku Bingwa wa Capital One Cup huanzia Raundi ya 3 ya Mchujo ya EUROPA LIGI.
Kwa kutwaa Capital One Cup Mwaka 2016, Man City watacheza Raundi ya 3 ya Mchujo ya EUROPA LIGI.
Ikiwa City watafuzu kucheza UCL kutokana na kumaliza ndani ya 4 Bora ya BPL au kutwaa Kombe la UCL, basi nafasi yao kucheza EUROPA LIGI itatwaliwa na Timu nyingine ya BPL kama inavyoelezwa chini:
-Kumaliza Nafasi ya 4 kwenye BPL kutawezesha Timu kucheza EUROPA LIGI ikiwa…
Manchester City watatwaa UCL na kumaliza nje ya 4 Bora ya BPL [Labda Liverpool wamalize Nafasi ya 4 ya BPL na pia kutwaa EUROPA LIGI].
-Kumaliza Nafasi ya 5 kwenye BPL kutawezesha Timu kucheza EUROPA LIGI ikiwa…
Manchester City hawatatwaa UCL.
-Kumaliza Nafasi ya 6 kwenye BPL kutawezesha Timu kucheza EUROPA LIGI ikiwa…
Manchester City wakimaliza ndani ya 4 Bora.
-Kumaliza Nafasi ya 7 kwenye BPL kutawezesha Timu kucheza EUROPA LIGI ikiwa…
Manchester United wakitwaa FA CUP na kumaliza ndani ya Timu 6 Bora na Man City wakiwemo ndani ya 5 Bora.
-Kumaliza Nafasi ya 8 kwenye BPL kutawezesha Timu kucheza EUROPA LIGI ikiwa…
Liverpool watatwaa EUROPA LIGI na kumaliza Nafasi ya 7 ya BPL na Man United kutwaa FA CUP na kumaliza ndani ya 6 Bora za BPL na pia Man City wakifuzu kucheza UCL ama kwa kumaliza ndani ya 4 Bora za BPL au kutwaa UCL.
-Klabu ambazo hazitaweza kucheza EUROPA LIGI…
Timu itakayofungwa Fainali ya FA Cup.
No comments:
Post a Comment