Saturday, 23 April 2016

MWAMBA MAMADOU SAKHO ACHUNGUZWA NA UEFA

 
Mchezaji wa eneo la ulinzi wa Liverpool mwamba Mamadou Sakho anachunguzwa na shirikisho la mchezo wa soka barani ulaya(UEFA)baada ya kufeli vipimo vya madawa ya kuongeza nguvu michezoni.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26,bado hajasimamishwa rasmi,hatajumuishwa kwenye kikosi cha Liverpool wakati uchunguzi wake ukiendelea,klabu ya Liverpool ilisema.
Sakho alinunuliwa kutoka PSG kwa ada ya pauni milioni 18 mwaka 2013,ameichezea Liverpool michezo 34 katika mashindano yote,timu yake inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya England inategemewa kuialika Newcastle United kwenye uwanja wa Anfield Jumamosi ya leo.

No comments:

Post a Comment