Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa Ligi ya Vodacom baada ya Jumamosi kuwafunga mabao 2-0, wapinzani wao wa jadi Simba
MECHI za raundi ya nne za Ligi ya Vodacom Tanzania bara zimeendelea tena wikiend iliyopita kwa timu zote 16 kushuka katika viwanja tofauti kusaka pointi tatu.
Mechi hizo zimebadili msimamo huo katika nafasi nne za juu lakini hata zile nafasi tatu za chini kutokana na baadhi ya timu kushuka na nyingine kupanda kuepuka janga la kushuka daraja.
Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa Ligi ya Vodacom baada ya Jumamosi kuwafunga mabao 2-0, wapinzani wao wa jadi Simba katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na washambuliaji Amissi Tambwe na Malimi Busungu, na kuipunguza kasi timu hiyo kutoka mitaa ya msimbazi baada ya kushinda mechi zao tatu mfululizo kabla ya kukutana na Yanga.
Mechi hizo zimebadili msimamo huo katika nafasi nne za juu lakini hata zile nafasi tatu za chini kutokana na baadhi ya timu kushuka na nyingine kupanda kuepuka janga la kushuka daraja.
Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa Ligi ya Vodacom baada ya Jumamosi kuwafunga mabao 2-0, wapinzani wao wa jadi Simba katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na washambuliaji Amissi Tambwe na Malimi Busungu, na kuipunguza kasi timu hiyo kutoka mitaa ya msimbazi baada ya kushinda mechi zao tatu mfululizo kabla ya kukutana na Yanga.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuendelea kuongoza Ligi ya Vodacom ikifikisha pointi 12 na mabao 11, ya kufunga huku yenyewe ikiwa imefungwa bao moja pekee katika mechi nne ilizocheza tangu kuanza kwa msimu huu.
Kwenye uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na klabu ya Azam FC, waliikaribisha Mbeya City, kutoka Jijini Mbeya na wenyeji waliweza kuutumia vyema uwanja wao kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Katika mchezo huo uliopigwa jana Jumapili mabao ya Azam yalifungwa na kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche huku bao la Mbeya City likifungwa na kiungo Raphael Alpha.
Matokeo hayo yameirudisha Azam FC, hadi nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 12 sawa na Yanga kufuatia kushinda mechi zote nne lakini ikiwa na idadi ndogo ya mabao ya kufunga na kufungwa .
Mabingwa wa mwaka 1999 na 2000 Mtibwa Sugar Jumamosi hii iliendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuwafunga Majimaji ya Songea bao 1-0, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wao wa Manungu Complex Turiani Morogoro.
Bao hilo la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa penati dakika za mwishoni na kiungo chipukizi Ally Shomari baada ya mshambuliaji wake Said Bahanuzi kuangushwa chini wakati akienda kufunga.
Ushindi huo unakuwa wanne mfululizo kwa Mtibwa Sugar inayonolewa na kocha mzawa Mecky Maxime, na imepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 112 sawa na timu za Yanga na Azam FC, tofauti yao ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba iliyopoteza mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Yanga imeshuka kutoka na nafasi ya pili hadi ya nne ikiwa imebaki na pointi zake tisa ilizozipata baada ya kushinda mechi zake tatu mfululizo kwa kuzifungwa timu za African Sport, Mgambo JKT na Kagera Sugar.
Timu ya Stand United iliyoanza vibaya kwa kupoteza mechi mbili ikiwa nyumbani uwanja wa Kambarage Jumamosi hii ilipata ushindi wake wa pili mfululizo ikiwa ugenini kwa kuifunga JKT Ruvu, bao 1-0, katika pambano lililofanyika uwanja wa Karume Dar es Salaam.
Ushindi huo ni faraja kwa kocha Patrick Liewig, ambaye tayari mashabiki wa timu hiyo walianza kuushinikiza uongozi kumtimua kutokana na kutofuraishwa na matokeo ya mechi za awali na kwa sasa timu hiyo imefikisha pointi sita na kupanda hadi nafasi ya tano.
Timu ya Majimaji ya Songea Jumamosi iliendelea kuwa na wakati mgumu katika mechi yake ya pili kucheza nje ya nyumbani baada ya kupoteza mchezo wa pili mfululizo kwa kufungwa na Mtibwa Sugar bao 1-0 na kujikuta ikibaki kwenye nafasi ya sita ikiwa na pointi zake sita.
Kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya timu ya Tanzania Prisons nayo ilipata ushindi wake wa pili mfululizo kwa baada ya kuifunga Mgambo JKT, bao 1-0.
Matokeo hayo yamerudisha yamerudisha matumaini kwa kocha Salum Mayanga, ambaye alipoteza mechi mbili mfululizo walizocheza ugenini.
Ushindi huo unaifanya Prisons, kufikisha pointi sita na kubaki nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kushinda mechi mbili mfululizo ilizocheza nyumbani dhidi ya wapinzani wao Mbeya City na hiyo ya Mgambo JKT.
Timu ya Toto African ikicheza mechi yake ya nne ugenini ilifanikiwa kupata pointi moja mbele ya wenyeji Kagera Sugar, katika pambano lililofanyika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora.
Sare hiyo inaifanya Toto kufikisha pointi tano na kupanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi hiyo baada ya kucheza mechi nne.
Timu ya Ndanda FC, ikicheza iliendelea kusuasua msimu huu baada ya jana Jumapili kupoteza mchezo wake iliocheza ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kufungwa bao 1-0 na African Sport.
Kipigo hicho kinaifanya Ndanda FC, kubaki kwenye nafasi ya tisa ikiwa na pointi nne katika michezo minne iliyocheza tangu kuanza kwa msimu huu.
Nayo timu ya Mwadui FC, Jumamso hii ilishindwa kutamba ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Coastal Union.
Matokeo hayo yanaifanya Mwadui FC, inayofundishwa na kocha Jamuhuri Kihwelo ‘Julio’ kubaki nafasi ya 10 ikiwa na pointi zake nne sawa na Ndanda FC.
Kwenye uwanja wa Ally Hasan Mwinyi Tabora wenyeji Kagera Sugar mambo bado hayajawa shwari kwao baada ya kulazimishwa sare wakiwa nyumbani na Toto Afrika ya Mwanza.
Matokeo hayo yameiacha Kagera kwenye nafasi ya 11 ikiwa na pointi nne kufuatia kushinda mechi moja dhidi ya Mbeya City na sare hiyo ya nyumbani.
Kwenye msimamo wa raundi hiyo ya nne Mgambo JKT, ya Tanga inashika nafasi ya 12, na hiyo inatokana na kupoteza mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Tanzania Prisons, uliochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kipigo hicho kimeiacha Mgambo JKT, kubaki na pointi zake nne sawa na timu za Coastal Union, Mbeya City,Ndanda FC na Mwadui FC.
Kikosi cha kocha Juma Mwambusi Mbeya City, kinashika nafasi ya 13, na hiyo imetokana na kupoteza mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Azam FC, mchezo ambao ulifanyika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mbeya City imebakiwa na pointi zake tatu ilizozipata kwa kuifunga JKT Ruvu kwenye mchezo wake wa raundi ya pili uliofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya.
Kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga African Sport jana Jumapili ilipata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi ya Vodacom baada ya kuifunga Ndanda FC, bao 1-0, matokeo ambayo yameitoa timu hiyo kwenye nafasi ya mkiani na kupanda hadi nafasi ya 14.
Ushindi huo unaifanya African Sport, kufikisha pointi tatu sawa na Mbeya City, katika mechi nne walizocheza ambapo wamepoteza tatu na kushinda moja.
Mabingwa wa mwaka 1988 Coastal Union mambo bado siyo shwari kwao baada ya kucheza mechi nne na kuambulia pointi mbili walizozipata kwa kupata sare mbili wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Mkwakwani.
Hayo siyo matokeo mazuri kwa kocha Jackson Mayanja, aliyekuwa akiifundisha Kagera Sugar msimu uliopita kutokana na usajili mzuri ambao wameufanya msimu huu kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 15.
Maafande wa JKT Ruvu mambo yamekuwa mabaya msimu huu kutokana na kupoteza mechi zote nne mfululizo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2015/16.
JKT Ruvu Jumamosi ilicheza kwa mara ya kwanza nyumbani uwanja wa Karume na kufungwa kwa bao 1-0 na Stand Unite jambo ambalo limeiacha timu hiyo kwenye nafasi ya mwisho ikiwa haina pointi hata moja ikijivunia bao lake moja ililolipata katika mechi dhidi ya Yanga.
No comments:
Post a Comment