Wednesday, 20 April 2016

Simba wahahidi Ubingwa lazima




TIMU ya Simba inaondoka keshokutwa Ijumaa kuelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na mechi dhidi ya  Azam itakayopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Aprili 30.
Simba imeshindwa kufanya vizuri katika michezo yake miwili iliyopita na kuwafanya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuanza kuwashutumu viongozi wao kuwa wanahusika na kuboronga huko kwa timu yao.
Mkuu wa kitengo cha habari na wasaliano wa klabu hiyo, Haji Manara amesema wanaenda Zanzibar kwa ajili ya kuandaa timu kwakua visiwani humo ni mahala tulivu ambapo wachezaji watapata muda mzuri wa kufanya mazoezi na kupumzisha akili.
"Ijumaa tunaenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kwa mechi yetu dhidi ya Azam ambayo tunaichukulia kwa umuhimu mkubwa kwa kuwa wote tunahitaji alama tatu kwa ajili ya kuchukua ubingwa," alisema Hajji.
Endapo Simba itapoteza mchezo huo itakuwa na nafasi ndogo ya kuchukua ubingwa baada ya kubakiwa na michezo mitano huku wapinzani wao Yanga na Azam wakiwa na michezo sita.
Wakatu huo huo kiungo Mwinyi Kazimoto amerejea mazoezini na wenzake baada ya kuumia alipokuwa akitumikia timu ya taifa ilipochez






No comments:

Post a Comment