Thursday, 21 April 2016

MAMBO KUMI YALIYOJITOKEZA BAADA YA YANGA KUTOLEWA NA AL HAALY

"ASANTENI KWA KUJA..... ILA CHA MOTO TUMEKIONA....."
MAMBO 10 NILIYOYAGUNDUA BAADA YA MECHI YA YANGA UGENINI:
1. HANS VAN DEL PLUJIM
kiukweli hapo zamani sikuwahi kumkubali huyu mzee hata kidogo kutokana na "unazi" niliokua nao kipindi hicho nadhani,ila kwa jana kani"prove" wrong na mawazo yangu "mgando", kuanzaia kikosi cha jana jinsi alivyokipanga na ile "Formation" aiseee kiukweli unastahili heshima mzee ni vijana wako tu wachache jana wamekuangasha... tumezoea mara nyingi timu zetu zikienda "ugenini" huwa tuna-defense tu na "vishambulizi" vichache sana vya kushtukiza,lakini jana "YANGA" kashambulia muda mwingi na mpira pia kaucheza japo haukuwa wa kiwango kikubwa sana. ‪#‎ShikamoBABU‬.
2. KAMUSOKO,DONALD NGOMA,BOSSOU,TAMBWE na HARUNA:
Kiukweli jana mmeonyesha nini umuhimu wa kuwa na "Maproo" wengi katika ligi yetu ya kibongo,bila ya uwepo wenu jana sidhani kama "YANGA" wangepata jeuri ile ya "ku-process" mpira atleast kwa muda hat wa dakika 3 hadi 4,lakini jana mpira ulipokua unakuja kwa "HARUNA" lazima kwanza atulize kisha aangalie mtu sahihi wa kumpasia,hali hiyo pia ilionekana kwa "NGOMA" na "KAMUSOKO" ila kwa "TAMBWE" kidogo jana katuangusha nahisi pengine ni kutokana na kukabwa sna,big kwa "DONALD" bonge la bao lile mwanangu.
3. JUHUDI BINAFSI ZA JUMA ABDUL:
Huyu "Mshikaji" majuzijuzi tu hapa niliwaambia anaujua mpira kweli kweli ila tatizo lake moja tu.. HASIRA na "BANGE" tu ndo vinamsumbua,mfano jana kaupiga mwingi mno,kateneneza "Bao" safi sana kwa "NGOMA",alichokifanya mbele ya yule beki wa AL AHLY ni juhudi binafsi tu,yaani huku kwetu tunaita "Kujiongeza" mshikaji alijiongeza alipoona hawezi kumwaga maji (kupiga krosi) ya moja kwa moja akaamua amfinye yule beki na kumwaga "kakrosi" kadogo tu kalikotua moja kwa moja kichwani kwa "NGOMA".. kwa tukio hili la jana mshikaji wangu JUMA hongera sana,hiyo ndio type ya beki namba mbili wa kisasa.
4. MBINU ZA ZIADA ZA MWARABU:
Ujue kiukweli "Mwarabu" alizidiwa "maarifa" kidogo na YANGA hasa ule muda wa kipindi cha pili baada ya kuingia lile goli,wakaanza kutafuta goli kwa nguvu,walipoona hawafanikiwi wakaanza kutumia mbinu za "ziada" kuwaaharibu YANGA "kisaikolojia" na hili walifanikiwa kwa asilimia kubwa tu,hasa lile tukio la "fujo" lililosababisha "NGOMA" kupata kadi ya njano,lile tukio sio la bahati mbaya aisee mkae mkijua lile tukio ni sehemu ya mipango yao wakishaonaga mambo magumu wanakuja na style ile,maara huyu kakupiga kibao,mara huyu kakutemea mate,mara huyu kakutia kidole yaani wanakufanyia visa vya kila aina ili mradi tu "upaniki" na kutoka kwenye mchezo,hili lilifanikiwa kwani baada ya YANGA kudili na soka sasa wakaanza kudili na fujo za mwarabu matokeo yake wakampa nafasi ya kujipanga upya kwa mashambulizi na muda mchache uliofatia wakapata goli. (how to be a professional)
5. KILIO CHA OSCAR JOSHUA....
Hivi kwanza unajua kwa nini "Oscar" alilia sna kwa uchungu baada ya kuingia kwa lile goli???jibu ni simpo tu,jamaa alicheza vyema sana hii game na sidhani kama kuna mtu alitegemea hilo... wengi waliamni huu ndo ungekuwa uchochoro wa "mwarabu" lakini UBAVU na UZOEFU vimembeba sana OSCAR jana,na mechi kama hizi uzoefu ni bora zaidi kipaji,namaanisha hivi HAJI MWINYI ana kipaji cha hali ya juu kumzidi OSCAR ila hana uzoefu wa game kubwa kama hizi kama unabisha hili juzi juzi tu tuliliona pale TANZANIA ilipokula WIKI kule ALGERIA,haji hakuwa mzoefu na jama mashambulizi mengi waliyatumia upande wake na walifanikiwa hilo,kwa hiyo jana kwa oscar alistahili kulia kwa kweli hata ningekua mimi ningemwaga chozi zile dakika zinauma sana bora ufungwe hata mwanzoni kiukweli.
6. REFA:
Kwa mara ya kwanza tangu nianze kuangalia mechi za "Waarabu' wakiwa kwao namuona "REFA" yupo "FAIR" kabisa na maamuzi yake uwanjani,kama kuna shabiki wa YANGA atadiliki kusema "Waarabu" wamebebwa nadhani huyo atakua kaangalia mpira kupitia "STAR TV" au kwenye simu ya mkononi,jana bhana kiukweli bin haki mwamuzi alikua yupo fair kwa maamuzi ya pande zote mbili.
7. CAPTEEEEIIIIIIN NADIRI:
Jamaa amezihirisha badi tunamuhitaji sana tu kwenye soka letu kibongobongo,jana ka-perfom vizuri tu,kautendea haki unahodha wake,naamini hata kule ALGERIA kwenye zile 7 kama angekuwepo basi zingepungua idadi,sio kwamba anacheza peke yake kwenye timu hapana bali anajua kuhamasisha wenzie ni mzoefu wa michuano ka ile pia,so jana tumeona alivyojitahidi sana kuhamasisha wenzie nini cha kufanya...‪#‎MKWASA‬ kama unanisikia huyu jamaa mtake radhi bado tunamuhitaji National Team aiseeeee.
8. WENGI WALISAHAU KUWA AL AHLY NI TIMU YA AINA GANI:
YANGA jana imekutana na timu bora na kubwa barani AFRKA,time yenye wadhamini zaidi ya 10,ina kikombe cha kila aina,ina uwanja wake wa mazoezi,ina vitega uchumi vya kuiongezea mapato,ina wachezaji bora na kocha bora,pasipo sahau ina "sapoti" kubwa nyuma ya mashabiki wake,so kuitoa timu kama hii yatakiwa ujipange kweli kweli na ujue mpira kweli kweli,bado TANZANIA tuna safari ndefu ya kufikia mafanikio makubwa katika hii michuano na hilo litachukua muda mrefu sana,kila siku tutakuwa tunafurahia kupanda ndege na kusindikiza wenzetu tu,mipango madhubuti inahitajika,viongozi wanaojua soka wanahitajika pale TFF na hizi timu za SIMBA na YANGA ifike mahala ziruhusiwe tu kuendeshwa na "boss" mmoja tu naamini,tutapata wachezaji bora wa kupambana huko siku za usoni.
9. TUNAHITAJI WALIMU WA "SAIKOLOJIA" KWENYE TIMU:
Kwa "YONDANI" Nahisi jana bado ile hali ya "ubaridi" ilikua inamsumbua na bado hajachanganya kwenda sawa na wenzie,maana kwa style ya lile goli lililofungwa mpigaji kichwa akitokea nyuma upande wake ilidhihirisha hili,mchezaji anatakiwa muda wote awe mchezoni aisee..na ndio maana timu zetu zinatakiwa kuwa na watu maalumu wa "saikolojia" mfano jana uliona yule namba 10 mgongoni wa "waarabu" kabla hajaingia alichokua anafanyiwa na yule kocha wao wa viungo???alikua anamuinua kila dakika anamuambia apashe misuli,anama ushauri wa hapa na pale,ile ndio inatakiwa hata kwenye vilabu vyetu..sasa kumbuka kabla ya "kelvin" kuingia nani aliketi ae chini na kumkumbusha wajibu wake??maana naamini wajibu wa kuingizwa kwa kelvin jana ni kwenda "kukaba" tu ila walau matokeo yabakie vile yaani 1-1 ile waende kwenye hatua inayofata lakini kilichofatia mtu aliyetumwa hiyo kazi ya kukaba ndio "kanya" yaani boko limetokea kwake.
10. GAME ZIISHIE NYUMBANI/ASANTENI KWA KUJA:
Kuna umuhimu wa kumaliza "MECHI" nyumbani,hivi kwa mfano jana YANGA ile game ya kwanza yaani home wangeshinda zaidi ya goli 2 unadhani nini kingetokea na ile "spirit" waliyokua nayo jana????jamani sio kuwa jana eti mwarabu kafanya makusudi zile 2-1,hapana jana alishikwa kimbinu kweli kweli na ndio maana hao wenyewe mpaka muda huu wanawaambia yanga kuwa "ASANTENI KWA KUJA...ILA CHA MOTO TUMEKIONA..." ni dhahiri kama tutakua tunamaliza game zetu nyumbani hizi za igenini zitakua ni kumalizia tu vita...somo kwa vilabu vyetu vyote nchini.
MWISHO KABISA:
YANGA hongereni kwa kupambana kiume ila kuna mtu hapa ananiambia eti afadhali mmetoka ili tujue kuwa TANZANIA kisoka bado sana hasa nyanja za kimataifa..anadai kuwa laiti kama tungepita jana..leo tungejiona tushamaliza kila kitu.
">.....MUNGU IBARIKI TANZANIA... MUNGU IBARIKI YANGA IRUDI SALAMA KUMALIZIA ‪#‎VIPORO‬ VYAKE VYA ‪#‎VPL‬..."
Follow na U-LIKE ‪#‎PAGE‬ yangu inaitwa "Kijiwe Cha Mastory" upate vitu mbali mbali vya kuelimisha na kufundisha pia.

King Gwajeson Gwaje's photo.King Gwajeson Gwaje's photo.

No comments:

Post a Comment