Sunday, 26 May 2019

Tetesi za Usajili Balani Ulaya

Man united waonekana wameshinda mbio za kumsajili Matthijs De Light baada ya kuchuana vikali na klabu ya Barcelona na wako tayari kutoa dau la paun million 70 na mshahara wa pauni laki 350 kwa wiki ,kiasi ambacho Barca hawakuwa na uwezo nacho na hawako tayari kulipa kiasi hicho

Pia source ya habari inasema Barcelona wameshindwa kulipa ada ya wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola kiasi cha pauni million 12 .Na Man United wamekubali kulipa hicho kiasi kwa wakala huyo

Pia kilichoongeza uwezekano wa mchezaji huyo kuamia Man united ni pale alipoonekana kulike picha ambayo ilitumwa na Rio Fredinand kwenye twiter

Friday, 13 January 2017

Diego Costa kutemwa kikosi kitakachoumana na Leicester city leo

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji nyota Wa timu ya taifa ya Spain na kilabu cha Chelsea Diego Costa ataukosa mchezo Wa Leo ambapo Chelsea watakuwa wageni dhidi ya mabingwa watetezi Leicester city. Imeripotiwa kutokea kwa kutoelewana au kugombana kwa mshambuliaji huyo na kocha anayekinoa kikosi icho Antonio Conte pamoja na fitness coach Julio Tous.

Diego Costa aliripoti kuwa na maumivu ya mgongo ila timu ya madaktari walipuuza malalamiko yake yaliyopelekea mshambuliaji huyo kugomea mazoezi huku kocha wake kuamua kuwa upande wa jopo la madaktari kuwa kinyume na maamuzi ya mshambuliaji huyo anayesifika kwa utata katika vitendo..

Aidha Uongozi Wa Chelsea umekataa kutoa taarifa yoyote juu ya kusambaa kwa suala la mshambuliaji huyo kutemwa katika kikosi kinachoanza Leo.


Ripoti hizi huenda zikachochea tetesi za mshambuliaji huyo kutaka kuondoka katika kilabu icho na kutimkia ligi kuu ya uchina ambapo kandarasi yake imekua katika uhitaji mkubwa licha ya Conte kutaarifu kuwa biashara kati ya kilabu icho na uchina imekwisha kwa sasa.

Diego Costa ameweka kambani mipira 14 na kusaidia upatikanaji Wa magoli mengine 5 ka



Sunday, 8 January 2017

Wayne Rooney afikia Rekodi ya mabao ya legendary Sir Bobby Charlton

Mshambuliaji nyota Wa kilabu cha Manchester United na timu ya taifa ya uingereza, Wayne Rooney sasa anahitaji bao moja kuwa mfungaji bora Wa muda wote wa timu hiyo baada ya jana kufikia record ya mabao 249 akiwa na jezi ya Manchester united hapo Jana katika michuano ya raundi ya 3 ya FA walipoumana na kilabu cha reading.

Awali Wayne Rooney amepita akivunja records za Dennis Viollet (179 goals), Jack Rowley (211 goals), Denis law (237 goals), na kwa sasa hakuna mchezaji mwingine amefunga mabao mengi zaidi take katika kilabu icho.

Saturday, 7 January 2017

Kwa nini nyota Aubameyang alihudhuria 2017 CAF awards ceremony akiwa na mavazi yasio Rasmi?

Nyota mshambuliaji Wa kilabu cha Borrusia Dortmund cha ujerumani na timu ya taifa ya Gabon juzi alihushuria hafla za utoaji tuzo za wachezaji nyota Wa afrika nchini Nigeria,Abuja akiwa amevalia mavazi ya "Bash" .

Hiyo ni kutokana na kupotelewa na mizigo yake alipotua katika airport ya Abuja. Pierre Emeric Subameyang usiku huo alishuhudia nyota wa Leicester city na timu ya taifa ya Algeria Riyaad Mahrez akitwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha kilabu chake kushinda taji la Bacleys premier league ya Uingereza.

Tukio hilo lilitokea ikiwa imebaki takribani wiki 1 kuanza kwa michuano ya mataifa huru ya Africa AFCON nchini Gabon.

Wenger akiri angeweza kumtumia kiungo Jack Wilshere kwa sasa

Manager Wa washika mitutu Wa London, arsené Wenger amekiri angeweza kumtumia kiungo mwingereza Jack Wilshere katika kikosi chake cha sasa kilichokumbwa na majeruhi.
Jack wilshere alipelekwa kwa mkopo Wa mda mrefu katika kilabu cha Bournemouth mnamo mwezi Wa August ambapo mpaka sasa ameonesha uwezo mzuri.

Arsenal kwa muda mrefu sasa inakosa huduma ya kiungo wake mahiri Santiago carzola pamoja na mfaransa fransis Coquelin ambaye atakosekana kwa takribani wiki nne.

Alipoulizwa kama angeweza kumtumia Jack kwa sasa alijibu "ndio ningeweza kumtumia sasa"

"Lakini kama angekua hajacheza match yoyote mpaka sasa pia asingekuwa tayari kucheza kwa sasa. Na mpaka sasa naona ilikua uamuzi sahihi kwake kuenda kukipiga Bournemouth kwa mkopo"


Wilshere ambaye amecheza michezo 17 (15 akiwa na Bournemouth) ni idadi kubwa kwake ya michezo tangu msimu Wa 2013-2014

Arsenal Leo inajitupa dimbani kukipiga na Preston North end katika michuano ya FA ya pale uingereza

angalia magori kumi bora ya scorpion kick