Saturday, 18 July 2015

YANGA YAPATA KICHAPO KAGAME CUP

Timu ya Yanga fc ya Dar es salaam leo jioni imewezwa kufungwa na timu ya Gorlmahia ya kenya kwa jumla ya mabao 2 kwa moja

mchezo huo ambao ulianza kwa kasi Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga goli ,baaada ya mchezaji wa gorlmahia beki Boniface Olochu  kujifunga kutokana na mpira uliopigwa mshambuliaji wa Yanga mzimbabwe DORNAD NGOMA

Hata hivyo goli hilo halikudumu sana kwani dakika kumi baadae golmahia walisawazisha goli hilo kwa mpira wa faulo iliyopigwa kiufundi na kuunganishwa vizuri na beki  Dirkir Glay wao wa kati na kufanya matokeo kuwa moja kwa moja hadi mapumziko

kipindi cha pili kilianza huku kila timu zote zikianza kucheza kwa taratibu zikijalibu kusomana lakini walikuwa ni gormahia ndio waliofanikiwa kufunga bao baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuokoa mpira uliokuwa unaelekea golini kwao na kupokonywa na mshambuliaji wa golmahia na kumchambua vizuri kipa wa Yanga Bartezh

baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kufanikiwa kupata penati ambayo hata hivyo beki wa Yanga ambaye ni nahodha wa timu hiyo nadir canavaro alishindwa kuuweka mpira huo kimiani , na penalt hiyo ilipatikana baada beki wa Golmahia kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

hata hivyo kunako dakika ya 25 Yanga ilipata pigo baada mchezaji wake tegemeo NGOMA kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatiwa kupata kadi ya pili ya njano

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Kpah Sherman dk69, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Salum Telela dk84. 


Gor Mahia; Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk89, Godfrey Walusimbi/Ronald Omino dk86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie Kagere na Michael Olunga.



matokeo mengine ni kama ifuatavyo

KMKM 1   TELEKOM FC 0

APR 1 HEEGAN 0

No comments:

Post a Comment