Thursday, 5 May 2016

African Lyon yaja kimataifa zaidi

Sh
Dr-Sulaiman-Al-Fahim-Port-001


Mfanyabiashara maarufu wa kiarabu 
Dk Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon
 ambayo itashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.

Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi alisema kuwa waliamua kumuomba
 Al Fahim kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika michezo hasa mpira wa
 miguu mbali ya kuwa mfanyabiashara bilionea katika nchi za Uarabuni na duniani kwa ujumla.

Kangezi alisema kuwa Al Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate
 Development ya Dubai na miaka ya nyuma alikuwa
 msemaji wa kampuni inayomiliki klabu tajiri duniani, Manchester City,
 Abu Dhabi United Group (ADUG). ADUG iliinunua Manchester City Septemba, 2008.

Pia Al Fahim alitaka kununua klabu ya Portsmouth ambayo ilikuwa inashiriki
 ligi kuu ya Uingereza, lakini mpango huo haukuweza kukamilika.

Kangezi alisema kuwa Al Fahim ataanza kazi rasmi Aprili 16 ambapo atatangaza timu yake ambayo
 atafanya nayo kazi katika kuibadili klabu hiyo na kuwa klabu bora Tanzania na bara la Afrika.

Alisema kuwa uwepo wa Al Fahim kutaifanya timu hiyo kuwa na
 uongozi bora wenye kujua uendeshaji wa
 kisasa katika masuala ya mpira kwa
 kuzingatia uzoefu wa mfanya biashara huyo mzoefu katika soka na michezo mengine.

“Haikuwa kazi rahisi Al Fahim kukubali kuingia kwenye uongozi wa klabu yetu, ila tunashukuru
 kwani alituelewa baada ya kukutana naye alipokuja hapa nchini kwa shughuli zake”, alisema Kangezi.

Alisema kuwa lengo lake ni kuona African Lyon inakuwa klabu ya mfano si tu kwa Tanzania
, hata kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Kangezi alisema kuwa mipango yao ya
 awali ni kuimarisha timu ya kwanza ili  iweze kufanya vyema
 katika mashindano ya ligi kuu na pia kuanzisha msingi mzuri wa timu za watoto.

“Dk Sulaiman ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Al Fahim Group na vile vile
 alikuwa mkurugenzi wa kituo cha Royal Football Fund (RFF) mbali ya kuwa
 mchezaji wa mchezo wa chesi, ameahidi kusaidia wachezaji chipukizi ili
 kuwawezesha kushiriki katika mpira wa kulipwa, tunaamini tutafika,” alisema.

No comments:

Post a Comment