Thursday, 5 May 2016

MAMBO YANAELEKEA KUMNYOKEA FARIDI MUSA

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.

 
Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, amesema kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.

 
“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

 
Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.

 




 












No comments:

Post a Comment